Bondia Francis Miyeyusho (kushoto)
akitunishiana misuli na Emilio
Norfat ambao watazipiga kesho Jumapili October 5 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mpambano wa raundi nane.
--------------------------------------------
MABONDIA
mbalimbali watazipiga siku ya Jumapili kwa ajili ya mpambano wa ubingwa ambapo
bondia kutoka mkoa wa Tanga Tanzania Alen Kamote 'Rasta'' atazipiga na Osgood
Kayuni wa Malawi kugombea ubingwa wa Dunia wa UBO kg 61.
Hiyo ndio siku ya
kufurahia kwa wakazi wa Tanga kwani mpambano huo pia uatasindikizwa na mapambano mengine ambapo bondia wa Dar es salaam Thomas Mashali atavaana na bondia kutoka
Moshi Alibaba Ramadhani kugombania ubingwa wa Africa wa UBO kg 72
Pia siku
hiyo kutakuwa na mpambano mwingine mkali kati ya bondia namba moja kwa
ubora katika uzito wake featherweight Fransic Miyayusho atakaezipiga naEmilio
Norfat ambaye nae ni namba mbili katika uzito huo
Mapambano hayo yaliyoandaliwa jijini Tanga na promota mkongwe nchini Ally
Mwazoa ambaye kwa hivi sasa analeta burudani ya masumbwi nchini kupitia Mwanzoa
Promotion
Siku hiyo pia
kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo
wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu
kamili katika mchezo
huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama
Floyd Maywether,
Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...