Katibu na Mwanasheria mkuu wa kampuni
ya ufuaji umeme ya IPTL, Bw. Joseph Makandege akiwaonyesha waandishi wa habari
(hawapo pichani) nakala ya hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya Tanzania
ikizuia benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Tanesco kuendelea
kuwabugudhi wamiliki wa IPTL na kuingilia uendeshaji wa mitambo yake. Kushoto
ni Meneja Rasilimali watu wa IPTL Bw. Aidan
Kaude.
·
Yasema Bw. Sethi kuendelea kusimamia mitambo ya
ufuaji umeme ya Tegeta.
Mahakama Kuu ya Tanzania imeiamuru
Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Shirika la Usambazaji Umeme
Tanzania (TANESCO) kuacha kuingilia utulivu,
umiliki,
usimamizi
na utawala wa Mitambo ya ufuaji umeme ya Bw. Harbinder Singh Sethi iliyopo Tegeta, na kusubiri
uamuzi wa
mwisho wa kesi
yao ya
msingi.
Kampuni ya Independent Power
Tanzania
Limited
(IPTL) na Pan
African Power
Solutions
Limited
(PAP)
zilifungua kesi kwa kuhoji uhalali
wa maamuzi
ya Kituo
cha Kimataifa cha Kutatua
Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) dhidi ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) na Martha Renju (anaedaiwa kuwa
msimamizi wa mali zake), ijulikanayo kama "Decision
on Jurisdiction and liability" iliyotolewa katika
kesi ya ICSD
namba ARB
/ 10/20.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...