DSC_0177
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo (kulia) akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (wa pili kulia) kuzungumza na wakazi wa wilaya ya Uvinza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM mkoani Kigoma. Kutoka kushoto ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
 
Na Mwandishi wetu, Uvinza - Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya amesisitiza uadilifu katika vyombo vya habari jamii kwa kutangaza habari zisizoumiza hisia kwa wananchi wengine na kuepuka migogoro.
Akizindua kituo cha redio jamii cha Uvinza FM, Luteni Kanali Mstaafu Machibya alisema kuwa vyombo vina wakati mgumu hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Changamoto hii inaweza kuepukika kwa kuhakikisha habari zinazotolewa zinalenga kuendeleza utamaduni wa amani, upendo, utulivu na uvumilivu na kuepuka viashiria vinavyoweza kusambaza chuki kwa lengo la kufanikisha chaguzi salama.

Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza umuhimu wa kuutumia uhuru wa kutoa na kupata habari vizuri kwa kusema kwamba uhuru huo usitumike kutoa habari zinazopendelea upande mmoja na kukandamiza mwingine kwa kuwa hali kama hiyo husababisha machafuko.

“Kwa mujibu wa Ibara ya 18 (b) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi, lakini haki hiyo iende sambamba kwa kuzingatia Sheria za nchi na kuhakikisha habari hizo haziumizi hisia za wananchi wengine,”
DSC_0206
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisoma risala wakati wa uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM ambapo alilipongeza shirika la UNESCO kwa juhudi kuwaweka karibu wananchi na serikali kupitia mawasiliano ya redio.

Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya ameitaka redio jamii Uvinza kuonyesha uwezo wao ili waweze kujitangaza na kujijengea imani kwa wanajamii wao kuwa wanaweza. “Ni kwa hali hiyo tu mtaweza kujulikana, kutambulika na kupata udhamini na matangazo ya kutosha.”
Amewataka wanajamii kukitumia vyema kituo chao cha redio ili kiwe chachu ya kuleta na kukuza maendeleo katika vijiji, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...