Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akipiga kura leo kwenye ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kupitisha Sura na Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru pamoja Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo na Mhe. Mansoor Shanif Hiran, ambaye pia ni mbunge wa Kwimba (CCM).
Nadhani kuna huelewa mdogo kati ya wajumbe...mwanasheria mkuu was zanzibar ametimiza wajibu wake was kupiga kura kama wengine...au ndo kusema kura za ndio ndo kura sahihi? Leo ana one kana sio lolote ila kesho......! Mwanasheria asukumwi na majority..bravo
ReplyDelete