Kufuatia kifo cha Rais Michael Chilufya Sata, kilichotokea tarehe 28 Oktoba 2014, mjini London, na kwa kuzingatia Katiba yake Kifungu cha 38 (1) kinachohusu mamlaka ya Rais, kwamba nafasi ya Rais ikiwa wazi kwa sababu yoyote ile, Makamu wa Rais atakaimu madaraka ya kiti cha Urais hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika ndani ya siku tisini (90), hivyo Serikali imemteua Mhe. Guy Scott (MB), Makamu wa Rais, kukaimu nafasi hiyo katika kipindi hiki cha mpito.
Tayari aliyekuwa anakaimu madaraka ya Urais, Mhe. Edgar Lungu (MB) ameshamkabidhi madaraka hayo.
Hadi sasa kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, bado haijafahamika maombolezo rasmi yataanza lini na kwa siku ngapi au mazishi yatafanyika lini. Haya yote yanategemea maamuzi ya kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho kinakutana hivi sasa.
Hizi ni taarifa tunazoendelea kupokea, hivyo nasi tutaendelea kuwataarifu kwa kadri tunavyozipata.
UBALOZI , LUSAKA , ZAMBIA
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kusononeshwa sana na taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Michael Chilufya Sata ambacho kimetokea jana, Jumanne, Oktoba 28, 2014 kwenye Hospitali ya King Edward VII, London, Uingereza, ambako alikuwa anatibiwa akiwa na umri wa miaka 77.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kusononeshwa sana na taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Michael Chilufya Sata ambacho kimetokea jana, Jumanne, Oktoba 28, 2014 kwenye Hospitali ya King Edward VII, London, Uingereza, ambako alikuwa anatibiwa akiwa na umri wa miaka 77.
Katika
salamu ambazo amempelekea Makamu wa Rais wa Zambia, Mheshimiwa Dkt. Guy Scott
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Kikwete
amesema:
“Nimepokea
kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi, habari za kusikitisha za kifo cha
Mheshimiwa Michael Chilufya Sata, Rais wa Jamhuri ya Zambia. Kwa niaba ya
Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hakika, kwa niaba
yangu mwenyewe, napenda kukutumia wewe Mheshimiwa salamu za rambirambi za dhati
ya moyo wangu, na kupitia kwako familia ya wafiwa na ndugu wa Hayati Rais Sata
pamoja na Serikali na ndugu zetu wananchi wote wa Zambia kufuatia msiba huu wa
ghafla.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Hayati Sata atakumbukwa daima kama mmoja wa viongozi wa mfano wa kuigwa
katika Afrika. Katika kipindi chake kifupi cha uongozi wa juu wa Zambia,
alifanikiwa kuleta mageuzi makubwa katika maisha ya wananchi wengi wa Zambia.
Atakumbukwa pia kwa imani yake isiyoyumba ya kupigania uhuru, haki na usawa,
sifa ambazo zilimfanya kiongozi mpendwa ndani na nje ya mipaka ya Jamhuri ya
Zambia.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Hivyo, huyu ni kiongozi ambaye siyo tu atakumbwa na wananchi wa Zambia
lakini atakumbukwa na sisi sote wenzake na watoto wote wa Afrika.”
“Katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi na huzuni, tunaungana nanyi kuomboleza na
kumwomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na subira wana familia ya wafiwa, jamaa na
ndugu zetu wote wa Zambia ili waweze kuhimili machungu ya kipindi hiki cha
msiba mkubwa. Aidha, tuko pamoja nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke
pema roho ya Marehemu Michael Chilufya Sata.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
29 Oktoba,2014.
waafrika watu wapole sana. weusi kupata hata uongozi wa mtaa ulaya hakuna. ila sisi hatuoni tatizo kwa wazungu, wahindi, warabu, na baadaye wachina kushika nafasi nyeti za uongozi wa nchi.
ReplyDeleteupole wetu ndo ulifanywa tukawa watumwa na kukolonishwa.
we wacha ubaguzi huo,mbona weusi wengi tu ni viongozi ulaya na uarabuni .
ReplyDeleteakili finyu,
Wapo wakenya, wakongo, walioshika nafasi za uongozi ulaya, gombania kama unakidhi taratibu zao. Mzambia mweupe kama kakubalika sisi ni nani tumseme?
ReplyDeleteMawazo yako yamepitwa na wakati!
ReplyDeleteObama mjaluo USA
Monem Mwarabu Ex president Argentina(Marekani ya kusini).
Watu wanachagua kiongozi anayefaa sio ngozi au kabila au dini inabakia longolongo miaka 5 maendeleo nyuma miaka 100
Si kweli mbona obama mkenya anatawala marekani wapo wengi wanaongoza mitaa ulaya tuacheni ubaguzi
ReplyDeleteNakubaliana nawe, pengine usemayo yana kina. Lakini ningependa kukukumbusha kuwa the most powerful man in this planet at this moment ni mmatumbi, hivyo the future will possibly be different.
ReplyDelete