DSC_0209
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Jaji Francis Mtungi na kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na Nyuma kabisa ni Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza.
DSC_0232
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alipomtembelea leo na kufanya nae mazungumzo juu masuala mbalimbali ya maendeleo likiwemo suala la elimu na changamoto zake katika mkoa wa Dodoma.
DSC_0237
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph, Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza walipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...