Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile ambaye ndiye Mgeni Rasmi katika Mkutano wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wanaoishi nyanda za Juu kusini waliowahi kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka 1965-2014 na yeye akiwa ni mmoja wa wanafunzi ambaye alisoma katika chuo hicho mwaka 1967 na ambaye pia alikuwa ni Mkufunzi katika chuo hiki na Mlezi wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za juu kusini akitoa hotuba yake ambapo, alikishukuru chuo cha CBE kwa kufanya mkutano huu muhimu wa kuwaalika wahitimu wote kukutana pamoja pia aliongeza kuwa CBE ni chuo cha Kuigwa kwa sababu hata Viongozi baadhi yao Tanzania wamesoma katika Chuo hicho mfano Omar Kingi Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Stagomena Tax Katibu Mtendaji SADC, Harry Katillya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Suzan Kaganda-RPC Tabora, Dkt. Ramadhani Dau Mkurugenzi Mtendaji NSSF na Graciano Kanzugala Mwenyekiti wa TCCIA kanda za nyanda za juu Kusini , Alimalizia kwa Kuzindua umoja huo wa wanafunzi na kusema CBE ni chuo ambacho kimezalisha wataalam wengi . Mwisho alizindua Rasmi Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu kusini mkutano uliofanyika Tarehe 4.10.2014
Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile akisaini kitabu cha wageni wakati akiingia katika Mkutano huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...