MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo la Shams, jijini hapa.

Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari jingine katika eneo la Mbauda wakati akitokea katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.

Alifikwa na mauti katika tukio lililotokea kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku, ndani ya baa maarufu ya Arusha Raha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mroki alifika katika baa hiyo baada ya kufanikiwa kuwatishia kwa risasi waendesha bodaboda waliokuwa wamemzingira katika eneo la ajali na kisha kuondoka kwa kasi kwa gari lake aina ya Nissan Navara. 

“Alipiga risasi mbili hewani waliokuwa wamemzunguza wakanywea, akatumia mwanya huo kukimbia na moja kwa moja akafika Arusha Raha pengine kwa lengo la kujificha, na hapo akaanza kunywa…

“Ingawa inaonekana alikotoka alikunywa kidogo, alipofika Arusha Raha alikunywa haraka pombe mbili kali aina ya Valuer na wakati anamalizia ya tatu, akajikuta anazingirwa tena na wale waendesha bodaboda,” anasema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa, baada ya kufyatua tena risasi mbili nyingine hewani, lakini bila ya dalili ya watu hao kutishika, ndipo akaamua kujimiminia risasi.

Habari zaidi zinasema wakati anazingirwa, naye akijihami kwa risasi wasamaria wema wakiwa harakati za kupiga simu polisi walishitukia polisi wakiingia katika eneo la tukio lakini tayari Mroki alikuwa ameshajitoa uhai baada ya kujimiminia risasi kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusa Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa tukio, lakini chanzo chetu kikikataa kutajwa jina gazetini kwa kuwa si wasemaji wa matukio ya jeshi hilo mkoani Arusha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wataalamu wa magonjwa ya akili na wana saikolojia wafungue mjadala kuhusu hili swala la watu kujiua pengine tunahitaji simu maalum kusaidia watu kupata ushauri nasaha ili wasijimalize kabla ya muda wao.

    ReplyDelete
  2. Maajabu haya jamani

    ReplyDelete
  3. Mimi sina saykologia ya namna yeyote. Nionavyo mimi ni jamaa yetu jina lake pombe kumpunguzia mtu logic.He was feeling guilty after the first accident, kisha akazungukwa na wanabodoboda kama fisi wanavyomzunguka simba aliyeumia.Sikuwepo, lakini pengine walikuwa wapiga honi na kumzomea. Jambo kubwa ni kwamba hakumchukua mmoja wao katika safari yake.

    ReplyDelete
  4. RIP Brother Mroki. Wana SHISESCO wanakukumbuka sana.

    ReplyDelete
  5. Naona serikali inabidi iangalie upya utaratibu wa watu kupewa umiliki wa silaha! Inabidi watu wafanyiwe uchunguzi mbalimbali ikiwemo uchunguzi wa akili kabla ya kumilikishwa silaha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...