JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
AFYA NA USTAWI WA JAMII
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA MKOANI KILIMANJARO
Utangulizi
Mnamo tarehe 22 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa
kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwepo kwa mgonjwa
aliyehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu mwanaume ana umri
wa miaka 37, na mkazi wa Dar es salaam (Kimara ) ambaye
alikwenda Kilimanjaro tarehe 20 Oktoba 2014 katika kijiji cha Kirua kwa ajili
ya kusalimia ndugu. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali ( 38.2 0c), maumivu
ya Misuli, kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na maumivu ya koo na kupoteza
hamu ya kula.
Mgonjwa huyu anatibiwa katika Kituo cha Afya Shirimatunda,
Kilimanjaro kuanzia tarehe 22.10.2014 ambako yupo hapo hadi sasa. Mgonjwa huyu
kikazi ni “Land Surveyor” na hufanya kazi zake nchini na nje ya nchi ikiwemo
nchi ya Senegali. Mnamo siku za karibuni alikwenda nchini Senegali kwa kazi za
mkataba na kurejea nchini mwanzoni wa Oktoba 2014. Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi
zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola yaani Liberia, Guinea au Sierra Leone.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...