NA RIPOTA WA GLOBU YA JAMII
MWANASHERIA, Damas Ndumbaro ameingia kikaangoni baada ya kuitwa kwenye kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kujibu tuhuma alizozitoa wiki iliyopita.
Barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imemtaka Ndumbaro kufika kwenye ofisi TFF zilizopo jengo la PPF Tower leo saa 8:00 mchana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo tuhuma alizozitoa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.
Ndumbalo ambaye ni mwanasheria wa klabu za Ligi Kuu wiki ilitoa tamko kwa niaba ya wateja wake kuhusiana na makato ya asilimia tano ya wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Vodacom na Azam Media.
Kwa upande wake Ndumbaro alisema TFF ya sasa inamfanya kushuhudia maajabu makubw amabyo hayajawahi kutokea Duniani ya Wakili kushitakiwa kwa kosa la kumtetea mteja wake.
“Hii ni mara ya kwanza katika historia ya dunia hii Wakili anashitakiwa kwa kuwatetea wateja wake. Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni,” alisema Ndumbaro.
Aliendelea kufafanua kuwa uwakili ni kazi yake na ataendelea kutetea vilabu kwa nguvu zote mpaka haki sio tu itendeke bali ionekane kuwa inatendeka.
Hata hiyo aliitaka TFF kuanisha makosa yake kwa uwazi nasi kumuita tu bila kujua anakwenda kujibu nini na aliwata kusogeza mbele kikao hicho hadi Novemba atakapotejea nchini kwa kuwa hivi sasa anakwenda nchini Marekani kwa safari ya kikazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...