Mkuu wa Idara ya
Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) bw. Daniel Mafie
akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio
yaliyofikiwa na Baraza hilo ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika usajili wa
watahimiwa na uchakataji wa matokeo ya Mitihani ya Taifa. Kulia ni Afisa Habari
wa NECTA John Nchimbi.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la
Mitihani la Tanzania (NECTA) Bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari
leo jijini Dar s salaam kuhusu utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa
watahimiwa waliopoteza vyeti vyao ambapo utaratibu huo unahusisha uchunguzi wa
uhalali wa mwombaji. Kulia ni Afisa Habari
wa NECTA John Nchimbi na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la
Mitihani la Tanzania Bi Glee Magemba.
.Baadhi ya
waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
na Vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuonyesha mafanikio ya Baraza hilo nchini.(Picha na Frank
Mvungi-MAELEZO).
Frank- Mvungi - MAELEZO
Baraza la Mitihani la
Tanzania (NECTA) limedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa Mitihani ya
Taifa na udanganyifu wakati wa Mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu nchini.
Mafanikio hayo yametokana
na ushirikiano uliopo kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani katika
ngazi za mikoa na wilaya ili kutatua tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na
udanganyifu wakati wa mitihani uliokuwa ukifanywa kinyume na taratibu za baraza
la mitihani.
Hayo yamesemwa na Mkuu
wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo Bw. Daniel Mafie wakati wa mkutano
na waandishi wa habari leo Jjijini Dar es salaam uliolenga kueleza mafanikio
yaliyofikiwa hadi sasa.
Akifafanunua Mafie
amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 watahimiwa
waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na watahiniwa
9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.
Aidha Mafie aliongeza
kuwa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo
kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka
2012 na 3,303 mwaka 2011.
Akieleza zaidi kuhusu
mafanikio yaliyofikiwa Mafie alisema Baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya
Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika
matokeo ya mitihani ya Taifa.
Katika kukabiliana na
tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa
kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka
2008/2009 Baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa
katika vyeti vyao.
Katika utaratibu huo
vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalam hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa
na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au
kutumia vyeti vya watu wengine.
Baraza la Mitihani la
Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya
mwaka 1998 na 2002 kwa ajili ya
kuendesha mitihani ya Taifa kwa lengo la kuweka misingi ya sera ya mitihani,
kuendesha mitihani na kutunuku stashahada mbalimbali na vyeti kwa watahiniwa
wanaofuzu na kufaulu mitihani iliyo chini yake kisheria.
Udhibiti huu ni muhimu kwa sababu mtahiniwa yoyote anayetegemea njia za wizi kufaulu anajidanganya na anahujumu zoezi zima la kupima uwezo wake wa kuelewa.
ReplyDelete