Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana ( Mb) akizungumza hapo siku ya Ijumaa wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliokuwa ukihitimisha Wiki ya Afrika ambayo hufanyika kuanzia Octoba 13 na kuhitimishwa Octoba 17 ya kila mwaka. ni Wiki ambayo Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na washirika wengine wa Maendeleo huitumia kujadiliana, kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala muhimu ya kijamii, kiuchumi, kimaendeleo pamoja na hali ya amani na usalama. Vile vile hujadiliana mafanikio ya utekelezaji wa masuala hayo muhimu pamoja na changamoto mbalimbali ambazo bado zinalikabili Bara hili na namna ya kuzitafutia ufumbuzi.
Mhe. Pindi Chana ( Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akiwa na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...