Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wakazi wote wa Mkoa
wa Tanga ambao wanaendela na zoezi la ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili kwa
awamu ya kwanza kuwa, Serikali imesikia kilio cha wananchi wake na hivyo inapenda
kuwajulisha watendaji wote wa Serikali za mitaa ambao ndio wasajili kufungua vituo vya
usajili saa 1.30 na kufunga saa 12.00 jioni.
Kwa kuwa zoezi hili lilitakiwa kukamilika tarehe 17/10/2014, Serikali imeongeza siku
za usajili kwa lengo la kuweza kuwasajili wananchi wote ambao hawajasajiliwa. Aidha,
wananchi wote wanaoweza kujaza fomu za Utambuzi na Usajili, waruhusiwe kuzijaza na
msajili aweze kuzihakiki fomu hizo mbele ya mwombaji.
Kwa taarifa hii, Serikali inawahakikishia wananchi wote wa mkoa wa Tanga kuwa, wote
watasajiliwa na hivyo inawaomba wote ambao hawajasajiliwa wajitokeze na kuwahi vituoni
mapema kwa ajili ya kukamilisha zoezi la usajili wao. Napenda kuwahakikishia kuwa kila
mtu mwenye stahili ya kusajiliwa atasajiliwa na kuwa kitambulisho cha Taifa ni haki ya
msingi ya kila raia, mgeni mkaazi na mkimbizi mwenye umri wa miaka 18 na zaidi.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Imetolewa na:-
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...