Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam imezuia kufanyika kwa tamasha lililopewa jina ‘Bang Bang Bear Fest’ lililokuwa linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii.

Uamuzi wa mahakama hiyo umetokana na malalamiko yaliyotolewa na Bongo5 Media Group ambao wanamiliki wazo halisi la tamasha la aina hiyo liitwalo Dar es Salaam Bear Fest.

Kwa hali hiyo mahakama hiyo imetoa amri ya kusitishwa mara moja kwa ‘Bang Bang Bear Fest’ lililokuwa lifanyike October 4 kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam pamoja na kulipa hasara yoyote iliyotokana na kuingiliwa kwa haki miliki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Gharama za ku - copy na kupaste bila kuchanganya na akili zako kidogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...