![]() |
Marehemu Meja Jenerali (mst.) Aidan Isidore Mfuse |
Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse
(mstaafu) kilichotokea tarehe 29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini
India alikokuwa akipata matibabu.
Mwili wa
marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili
Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali
kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi
wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa
4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa
mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.
Imetolewa
na Kurugenzi ya
Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P
9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...