Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani.
Katika ujumbe wake wa siku ya makazi mwaka huu Waziri Tibaijuka ameviagiza vyombo vinavyohusika na upangaji miji kuongeza zaidi kazi ya upimaji wa makazi na kisha kuyaboresha makazi yaliyokwishavurugika kwa hivi sasa kwa mujibu wa takwimu za UN HABITAT, robo ya idadi ya watu wanaoishi mijini kote duniani na Tanzania ikiwamo wanaishi katika mitaa duni ambayo yana mazingira hatarishi, huku hali ya maisha ikiwa yenye uhaba wa huduma muhimu, ujumbe wa mwaka huu ni "Sauti kutoka Makazi Duni"
Waziri Tibaijuka ameziagiza Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya kujenga nyumba angalau 100 kwaajili ya wafanyakazi wake ili kwanza kupanga mij, lakini pia kupunguza tatizo la makazi holela yanayoikabili nchi kwa sasa. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
Tunashukuru NHC kwa kujenga nyumba za bei nafuu ila tunaomba muangalie wale mnaowauzia sio walengwa nina ushaidi wa nyumba mlizozijenga Arusha wamezinunua matajiri ili baadae watupangishe kwa bei kubwa, wale tuliopeleka maombi yetu tumebaki kuzitazama tu tetesi zilizopo ni kwamba hata bado nyumba kukamilika watu wameshapewa Mkurugenzi jaribu kuliangalia hili ili nasi tufaidike mana sisi ndo wenye shida nazo
ReplyDelete