Bw. Martin Kobler, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Misheni ya Kulinda amani katika DRC ( MONUSCO) akiwasilisha taarifa kuhusu MONUSCO mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo siku ya jumatatu. Katika maelezo yake Bw. Kobler amesema walinzi wa amani hawapaswi kukaa na kutochukua hatua au kuanza kuuliza maswali badala ya kuwakabili waasi wenye silaha ambao wanaonekana dhahiri kutishia usalama wa raia au hata usalama wao wenyewe. Na kwa sababu hiyo amewataka kutumia mamlaka na nguvu waliyopewa kwanza na kisha maswali yaulizwe baadaye.
Home
Unlabelled
PIGA KWANZA MASWALI BAADAYE-UMOJA WA MATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...