Moja ya kitu ambacho Jeshi la Polisi nchini limecheza heko,ni kuanzisha kitengo cha Ulinzi shirikishi kwa kuwachukua vijana mbali mbali mitaani na kuwafunda vyema baadhi ya kazi za jeshi hilo vijana wa Polisi Jamii,hiki ni kitu kikubwa na safi sana kwa vijana hao kwa wingi wao,kwani wameweza kulipiga tafu Jeshi hilo,hasa katika kusaidia Askari wa Usalama Barabarani kuongoza magari ili kupunguza misongamano isiyokuwa na ulazima.pichani ni mmoja wa Polisi Jamii akiongoza magari barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hata mimi nawapongeza sana kwa hilo ila kuna tatizo moja nalo ni "JE NANI ANAWALIPA?"
    Sababu ya kuuliza hivi ni kuwa sehemu nyingine wamekuwa ni tatizo sababu hawana mishahara hivyo wanasumbua watu pamoja na kuomba / kulazimisha rushwa toka kwa wananchi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...