Msomi maarufu nchini Kenya na Afrika Mashariki,Prof. Ali Alamin Mazrui (pichani) amefariki dunia leo asubuhi Binghamton Jijini New York nchini Marekani.
Prof. Mazrui amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81,taarifa za awali zinaeleza kuwa Prof. Mazrui hakuwa akijisikia vizuri kwa miezi kadhaa kabla ya kifo chake.
Mwenyekiti wa Haki za Binadamau za Waislam (MUHURI) Khelef Khalifa amesema mwili wa marehemu Prof. Prof Mazrui utasafirishwa kwa ndege kwenda Kenya kwa mazishi.
Binghamton si jijini New York. Ni mji wa New York State huko Up State kuelekea Syracuse na Bufallo.
ReplyDelete