Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa jengo la hoteli ya Gold Crest linalomilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.Wengine pichani toka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo,Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PPF,ndg. Ramadhan Kijjah,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Adam Malima,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PPF,William Erio pamoja na Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufuli.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli linalomilikiwa na Mfuko wa PPF jijini Mwanza.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PPF Ndg. William Erio.
Naibu Waziri wa Fedha,Mhe. Adam Malima (Mb) akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli inayomilikiwa na Mfuko wa PPF jijini Mwanza. Ufunguzi huo uliambatana na Rais kutembelea sehemu mbalimbali za jengo hilo la Hoteli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...