TIMU ya Taifa ya Safari Pool imeonyesha uwezo wa juu baada ya
kuzichapa timu za kombania za Mikoa ya kimichezo ya Ilala na Temeke
kwa siku tofauti katika kujiweka sawa na mshindano ya Afrika ya
mchezo huo yajulikanayo kwa “Safari All Africa Pool Championship”.
Timu ya Safari Pool ilianza mchakato wa kujipima ikiwa ni sehemu
ya maandalizi natimu ya Kombania ya Mkoa wa kimichezo wa Ilala
ambapo waliibuka na ushindi wa 12-9 katika mchezo uliochezwa Ijumaa
octoba 10,2014 kwenye Ukumbi wa Mashujaa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kutoka Ilala walikutana na timu ya Kombania ya Mkoa wa
Temeke Jumamosi Octoba 11,2014 katika mchezo ulichezwa katika
Ukumbi wa Mpo Afrika Tandika jijini Dar es Salaam na kuibuka na
ushindi wa 13-3.
Octoba 12,2014 timu itakutana pia na Kombania ya Mkoa wa kimichezo
wa Kinondoni katika mchezo unaotarajiwa kufanyika katika Ukumi wa
Face 2 Face uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa timu ya Taifa, Denis
Rungu alisema kikosi chake kiko safi na mchakato wa mechi za kirafiki
tatu za mikoa ya kimichezo ya Ilala, Temeke na Kinondoni ni semu
ya kupima kikosi chake lakini pia ni sehemu ya mchujo wa kupata
wachezaji 8 kutoka kundi la wachezaji 16 walioko timu ya Taifa.
Alisema Kocha timu inatarajiwa kuingia Kambini leo ambapo ndio
sehemu muafaka ya kujiandaa vema na mashindano ya Afrika kwa
mwaka 2014 ambapo Tanzania ndio muandaaji.
Mashindano ya Safari All Africa Pool Champonship yanatarajiwa
kufunguliwa rasmi Octoba 16 na kumalizika Octoba 18 ambapo mgeni
rasmi anayetarajiwa mkufungua mashindano hayo ni Waziri wa Habari
Utamaduni, Vijana na Michezo.
Nchi zilizothibitisha kushirika mpaka sasa ni mabingwa watetezi Zambia,
Afrka Kusini, Kenya, Cameroon, Lesotho, Malawi, Uganda na wenyeji
Tanzania.
Nahodha wa timu ya Taifa ya mchezo wa Safari Pool, Charles Venance akicheza wakti wa mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Kombaia ya Mkoa wa kimichezo wa Temeke uliochezwa katika Klabu ya Mpo Afrika Tandika mwishoni mwa wiki.Timu ya Taifa ilishinda 13-3.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool wakiwa na viongozi wa Mkoa wa kimichezo mara baada ya timu ya Taifa kibuka na ushindi wa 13-3 dhidi ya timu ya kombania ya mkoa huo iliyochezwa mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...