Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Pool Afrika (2014 All Africa BlackBall Pool Championsship) yanayotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Oktoba 16-18,2014 kwenye Ukumbi wa Burget,Kunduchi Jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yatashirikisha timu kutoka Zambia,Afrika Kusini,Malawi,Lesotho,Kenya,Uganda na Wenyeji Tanzania,ambapo mshindi wa jumla ataondoka na kitita cha Dola za Marekani elfu 5,huku wa pili akipata dola elfu 2.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa ambao ndio Waratibu wa Mashindano hayo,Amos Kafwinga.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Pool Tanzania,Dennis Lungu akieleza namna timu yake ilivyojipanga vyema kushiriki kwenye mashindano hayo,huku akijitamba kuwa ushindi lazima ubaki Tanzania,kwani anaiamini timu yake.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo na kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga.
Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa ambao ndio Waratibu wa Mashindano hayo,Amos Kafwinga akitoa shukrani nyingi kwa wadhamini wao ambao ni Safari Lager kwa kuweza kufanikisha mashindano hayo kufanyika hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...