Mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Bi Christina Innocent Marolen, almaarufu kama "Mama Bishanga", na mfanya kazi mwenzake kutoka Liberia wanonekana wakiwa kazini, Adern Court Alzheimer Home Care huko Ohio, Marekani, wakifurahia uamuzi wa madaktari watano wa Tanzania wanokwenda kuongeza nguvu ya kusaidia kuwatibu raia wa Liberia, baada ya kusoma taarifa hizo kwenye magazeti ya Tanzania.
Julie Blanton ambae alikuja Amerika miaka mingi mara baada ya vita iliotokea Liberia miaka ya themanini na tisini, huwa anenda kwao kila mwaka kusalimia ndugu zake.
Julie ameshukru sana Rais Kikwete na watanzania kwa ujumla kwa moyo wao wa upendo na kusaidia nchi nyingine tangia miaka sana iliopita katika nyanja mbali mbali, ikiwa ni pamoja na vita vya ukombozi barani Afrika. Kasema GOD BLESS ALL TANZANIANS.
Mama Bishanga (kulia) na shosti yake Julie pia wanawapa mkono wa herI ya kuzaliwa/ happy birth day mwanae Kenny @ Henrich na Rais Jakaya Kikwete, Bishop Desmund Tutu wa Afrika Kusini na wote waliozaliwa tarehe saba mwezi huu wa Oktoba. Kasema Mungu awaongezee upendo na nguvu ya kufanya kazi na kulitumikia taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...