Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Alhamisi na Iijumaa ya tarehe 30 na 31 Octoba 2014, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Chambezi, Bagamoyo. 

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe. Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.

        Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima. 

Au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja namba 022- 2194800 Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. 

Imetolewa na ofisi ya uhusiano, 
Dawasco - Makao Makuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kweli mkuu maeneo uliyo yataja ndiyo yenye maji ya bomba yakiyobakia kisimani kwenda mbele (bado wako stone age) Ukonga kweda juu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...