Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.
SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy.Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.





Jamani eeeh!kuna mambo mengi ya kuzungumzia kutatua matatizo ya watz badala ya mambo ya ngono. Mtu yeyote anaeanzisha mazungumzo kama haya,tuwaulize litatusaidiaje waafrika kwa magonjwa,njaa,umaskini wa mali na fikra,list goes on......
ReplyDeletePongezi kwa serikali yetu katika hili!
ReplyDeleteKepekee nachukua fursa hii kuipongeza sana serikali yangu ya Tanzania kwa kuweka bayana msimamo wa Watanzania kuhusu pendekezo hili la ushoga kujumuishwa kwenye malengo ya melenia. Kwa kipekee nampongeza mkurugenzi huyu wa idara ya ushirikiano wa kimataifa kwa umahiri mkubwa wa kuuelezea vema msimamo huo wa Taifa letu katika washa hii, MSG SENT.
Nafakiri ni vema mataifa haya yaliyoendelea yakaelewa kuwa sisi kama moja ya nchi za LDC's watu wetu wanakumbwa na dimbwi kubwa la umaskini ambao umekuwa ukizifanya serikali zetu za nchi za LDC's zihangaike usiku na mchana ili kuhakikisha watu wake wanaondokana na tatizo hili la umaskini. Ni muhimu kuelewa kuwa vipaombele vya nchi hizi sio ushoga ambao kimsingi si kinyume tu na maadili yetu ya kiafrika bali pia imani zetu zinazozizungaka jamii zetu.
Tungependa kuona mjadala wa malengo mapya ya melenia unajikita kwenye kutatua na kuboresha maisha ya watu duniani hasa wale wa ulimwengu wa tatu kwa kuwapa uhakika wa kupata elimu bora, huduma bora za afya, maji safi na salama uhakika wa kupata chakula kwa siku na malazi bora BADALA YA KUENDELEZA UKOLONI MAMBOLEO WA KUZINGAWANYA JAMII HIZI ZA KIAFRIKA KWA KUTUMIA DHANA HII YA USHOGA ambayo kimsingi inapingana na maadili yetu.