Msemaji wa tamasha la Karibu Music Festival, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. ..Wapo pia Prof. Jay, Barnaba, Shilole
Na Andrew Chale
WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mapema Oktoba 27, Msemaji wa tamasha hilo Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ alisema maandalizi yamekamilika na tayari wasanii wa awali waliopatikana wapo hadharani wanaendelea na matayarisho huku akiwaomba watanzania na wadau wa burudani kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.
Jazzphaa aliwataka baadhi ya wasanii wa nje na ndani na nchi zao katika mabano ni Panda (Japan), Maria Kate (Ufaransa), IFE Pianki (Uganda), Masayo (Japan), Fantuzz (Marekani), Shiwe Musique (Comoro), Dwembede (Kenya) na Mbiye Ebrima (Guinea).
Mwanamuziki wa Msafiri Zawose anayepiga nyimbo za Cigogo, akionjesha vionjo vya moja ya nyimnbo zake kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho kwa wanahabari.
Makundi na majina ya wasanii kutoka nyumbani ni pamoja na Afrikabisa Band, Wahapahapa, Segere Original, Jahazi, The Spirit Band na Mama Africa. Wengine ni Cocodo Band, Hokororo Band, Swanu Gogo Vibes, Swahili Vibes, Fimbo Band, Abeneko Music, Man Kifimbo, Saganda na Msafiri Zawose.
Wasanii wengine ni Msafiri Zawose ‘Chibite Zawose’, Tongwa Ensemble, Leo Manyika, Swahili Blues, Profesa Jay, Shilole, Juma Nature, Barnaba, Vitalis Maembe na Jhikoman. Aidha, Jazzphaa aliongeza kuwa lengo la tamasha hilo ni kukuza na kurasimisha tasnia ya muziki kwa umakini zaidi na kukuza uchumi wa eneo la Bagamoyo ambalo ni la kihistoria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...