Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujengewa uelewa wa mpango
wa kunusureu kaya maskini unaoratibiwa
na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TASAF kwenye
ukumbi wa TEC mjini DSM.
Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF,Bw. Alphonce Kyariga
(aliyesimama) akifungua warsha ya kuwajengea uelewa kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga maafisa ufuatiliaji TA wa mamlaka za utekelezaji PAAs kwa pya kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujengewa uelewa wa mpango
wa kunusureu kaya maskini unaoratibiwa
na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TASAF kwenye
ukumbi wa TEC mjini DSM.
Washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujengewa uelewa wa
Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiowa na TASAF wakiwa katika ukumbi
wa TEC mjini DSM kupata maelezo ya
mpango huo kabla ya kwenye katika maeneo ya utekelezaji katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Mwanza,
Shinyanga Na Simiyu.
Mmoja wa wawezeshaji wa warsha ya kujen gewa uelewa maafisa
ufuatiliaji wapya wa mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN
Bi.Woisso kwenye ukumbi wa TEC
mjini DSM .
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaanza awamu ya nne (wave
4) ya zoezi la kubaini kaya maskini
katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Morogoro, Tanga na Pwani Oktoba 6
Mwaka huu.
Katika maandalizi hayo TASAF imeanza warsha kwa ajili ya wawezeshaji
wa Kitaifa, wataalamu wa ufuatiliaji TAs na watumishi wa makao makuu (TMU)
ambao watakwenda kufanya kazi kwenye maeneo ya utekelezaji wa Mradi katika
mikoa hiyo.
Akifungua warsha hiyo
kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa TASAF
Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi wa uratibu wa TASAF Bw. Alphonce Kyariga amesema kazi ya utambuzi
wa kaya maskini ni nyeti na inayotakiwa kufanywa kwa umakini mkubwa ili
kupunguza uwezekano wa kutozibaini kaya za walengwa.
Amessistiza kuwa miongozo na taratibu zilizowekwa na TASAF
zinapaswa kufuatwa ili hatimaye zoezi
hilo liwe la mafanikio makubwa kama inavyotarajiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...