Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Katibu wa Klabu ya Ikulu Ramadhani Bendera ameipongeza klabu yake kwa kufanya vizuri katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi wa Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini morogoro. 
Bendera alitoa pongezi hizo kwa klabu yake kufuatia ushindi waliopata katika michezo mbalimbali iliyochezwa leo katika uwanja wa Jamhuri. 
Timu za Ikulu zilizofanikwa kuingia hatua ya robo fainali za mashindano hayo ni timu ya mchezo wa mpira wa pete, mchezo wa kuvuta kamba wanaume na ya wanawake. 
Katika mchezo wa mpira wa pete, timu ya Ikulu imewabwaga timu ya Ulinzi kwa magoli 52-10 na hivyo kuingia hatua ya robo fanali na kusubiria timu zitakazofuzu hatua hiyo. 
Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba, timu ya Ikulu wanaume imeibuka washindi kwa kuwavuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi 2-0 wakati timu ya wanawake ya Ikulu nao wameivuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa mizunguko yote miwili ambapo hadi mwisho wa mchezo Ikulu wameshinda 2- Mifugo 0. 
Aidha Bendera amesema kuwa maandalizi mazuri ya klabu yake na wachezaji kujituma ndio msingi wa ushindi wao wa leo kaatika michezo hiyo. 
Mashindano ya SHIMIWI nchini lengo lake kuwajengea watumishi afya bora na kujenga umoja wa kitaifa kupitia Wizara na mikoa mbalimbali ambapo michezo inawakujenga ari ya ushindani ndani ya watumishi wa umma na hatimaye kuleta ufanisi na tija kwa taifa wakati wakitekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
 Timu ya Ikulu ya kuvuta kamba wanawake wakiwa kwenye mechi za hatua ya timu 32 wakiwavuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwashinda kwa 2-0 wakati wa mashindano ya SHIMIWI taifa leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
 Timu ya Ikulu ya kuvuta kamba wanaume wakiwa kwenye mechi za hatua ya timu 32 wakiwavuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwashinda kwa 2-0 wakati wa mashindano ya SHIMIWI taifa leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Mchezaji Monica Kassy (GS) (wa kwanza kushoto) wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu akiwa amefanikiwa kufunga goli wakati wa mechi kati ya timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.

 Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu Rukia Kibayasa akimiliki mpira wakati wa mchezo dhidi ya Ikulu na Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.
Sehemu ya  ya mashuhuda wa mchezo wa mpira wa pete kati ya Ikulu na Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...