Na Georgina Misama-MAELEZO
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeiwezesha Serikali
kukusanya mrabaha wa jumla ya shilingi billioni 5.2 tangu kuanzishwa kwa
wakala huo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi uzalishaji na usafirishaji wa madini
Bwn Conrad Mtui wakati wa ziara ya waandishi wa habari walipotembelea migodi
ya Lugoba na Msolwa Chalinze, hivi karibuni.
“Wakala umefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 5.2 kutokana na
madini hayo yaliyozalishwa na kuuzwa na wamiliki halali wa leseni katika
mikoa mbalimbali kwenye kanda za Kaskazini, kati, Kusini, Kusini Maghalibi,
Maghalibi, Mashariki na Ziwa Victoria” alisema Mtui.
Aidha,Wakala kwa kushirikiana na Ofisi za Madini ulibuni matumizi ya “Hati ya
Mauzo” kwa lengo la kudhibiti shughuli za uzalishaji na mauzo ya madini, mkakati
ambao ulianza kutumika mwezi Juni, 2011 utakaohusisha Mikoa ya Dar es Salaam
na Pwani.
Pia, Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na
migodi mikubwa ya madini nchini, ikiwa na lengo la kupata mrabaha na takwimu
sahihi za madini yaliyozalishwa na migodi hiyo.
Akitaja migodi iliyofanyiwa ukaguzi alisema ni Mgodi wa dhahabu wa Geita,
Golden Pride, Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika
iliyowezesha kukusanywa kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 427.98
Akizungumzia kuhusu hatua wanazochukuliwa baadhi ya wamiliki wa migodi
wanaokiuka taratibu za “Hati ya Mauzo” Mkaguzi wa Madini ya Ujenzi na
Viwandani Abubakari Jihango alisema kuwa hadi sasa kuna kuna kesi 53
mahakamani, na kama itadhihirika ukiukwaji wa sheria, taratibu za kisheria
zitafuatwa.
Meneja wa Maabara kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) Mhandisi
Mvunilwa Mwarabu akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine
ya kupimia kiwango cha madini inayoitwa Atomic Absorption Spectroscopy
(AAS) walipotembelea Maabara ya Wakala huo jijini Dar es Salaam leo.
Mkemia Alfred Aloyce kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA)
akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sampuli ya jiwe la dhahabu
iliyotayarishwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara ili kubaini kiasi
cha madini ya dhahabu kwenye jiwe hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...