Na Happiness Shayo-Morogoro
Timu ya soka ya Uhamiaji imeweka historia katika michezo ya
SHIMIWI baada ya kuifunga timu ya soka ya Ikulu bao moja kwa bila
katika mchezo wa mtoano uliofanyika viwanja vya Morogoro Sec.
mjini Morogoro na hivyo kuitoa timu hiyo ya Ikulu katika mashindano
ya SHIMIWI.
Mchezo huo wa aina yake uliochezwa kwa vipindi viwili vya dakika
thelathini ulianza kwa kasi huku timu ya Ikulu ikijitahidi kushambulia
lango la Uhamiaji kupitia mshambuliaji wake Salehe Hamad bila
mafanikio.
Ikulu ambayo inaongoza kwa kunyakua kombe la soka la SHIMIWI
kwa mfululizo ilishindwa kufunga bao katika kipindi cha kwanza
cha mchezo huo hivyo hadi timu hizo zinaenda mapumziko hakuna
aliyemfunga mwenzake.
Uhamiaji iliyokuwa imeangukia kundi la wafungwa bora kwa kupata
pointi 4 katika michezo ya SHIMIWI ilijitoa kimasomaso katika kipindi
cha pili cha mchezo huo baada ya mshambuaji wake Edward Dafe
kufunga bao la kufuta machozi lililoiingiza timu hiyo katika 16 bora.
Goli hilo la Uhamiaji lilileta changamoto kwa wachezaji wa Ikulu
ambao mda wote walipania kunyakua ushindi na kupelekea
kucheza rafu hadi kumjeruhi kipa wa Uhamiaji Josia Steven ambaye
aliendelea na mchezo baada ya kupewa huduma ya kwanza.
Akiongelea mchezo huo Katibu wa timu ya Uhamiaji Bw.Richard
Mwasongwe alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwa timu yake
lakini jitihada binafsi zimepelekea kuwa na matokeo mazuri.
“Mchezo huu ni mgumu sana lakini timu yangu imejitahidi kadri
iwezekanyavyo kufanya vizuri” alisema.
Kwa upande wa timu ya Ikulu, ilishindwa kutoa ushirikiano wa
kuelezea hali halisi ya mchezo huo na badala yake kuondoka
uwanjani kwa majonzi.
Timu za soka zilizoingia 16 bora zitaingia dimbani Oktoba 6 ambapo
watakaofanikiwa kupita katika hatua hiyo wataingia robo fainali ya
mashindano ya SHIMIWI.
Timu ya soka ya Uhamiaji kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi yake na timu ya soka ya Ikulu (haipo pichani) katika mchezo wa mtoano wa SHIMIWI uliofanyika uwanja wa Morogoro Sec. mjini Morogoro leo.
Timu ya soka ya Ikulu ikifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mechi dhidi yake na timu ya soka ya Uhamiaji (haipo pichani) katika mchezo wa mtoano wa SHIMIWI uliofanyika uwanja wa Morogoro Sec.mjini Morogoro leo.(Picha zote na Happiness Shayo)
Sports clubs have been popular even in the past since sports teams of various sports need places to practice and enhance their sports skills....!!
ReplyDeletesports club la dc classes