Katibu na
Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege,
(mwenye suti nyeusi kushoto) akimkabidhi Mwinjilisti wa Kanisa la KKKT Usharika
wa Likamba Wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Bi Martha Musa Kivuyo (mwenye nguo
nyeupe), mfano wa hundi ya Shilingi milioni 10 kati ya Silingi milioni 20 (Tsh
20m/-) iliyotolewa na kampuni ya IPTL/PAP, kusaidia kwaya ya Patano la Usharika
wa Likamba kuweza kurekodi albam ya nyimbo za injili.
Katibu na
Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege,
(mwenye suti nyeusi kushoto) akipongezwa na Mdhamini na Mlezi wa kwaya ya
Patano la Usharika wa Likamba kanisa la KKKT la Arumeru, mkoani Arusha, Bw.
Philip Makini baada ya kukabidhi mfano
wa hundi ya Shilingi milioni 10 kati ya Silingi milioni 20 (Tsh 20m/-)
iliyotolewa na kampuni ya IPTL/PAP, kusaidia kwaya ya Patano la Usharika wa
Likamba kuweza kurekodi albam ya nyimbo za injili. Wakishuhudia ni Mwinjilisti
wa Kanisa hilo, Bi Martha Musa Kivuyo (mwenye nguo nyeupe), na Meneja Uhusiano
wa Jamii wa IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph pamoja na wanakwaya.
Katibu na
Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege,
(kulia) akizindua albam mpya ya nyimbo za injili ya kwaya ya Patano la Usharika
wa Likamba Kanaisa la KKKT la Wilaya ya Arumeru, Arusha. Kati kati ni Meneja
Uhusiano wa Jamii wa Makampuni ya IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph akifuatwa na
Bi.Hellen Zelothe.
Katibu na
Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege,
(kulia) akionyesha albam mpya ya nyimbo za injili ya kwaya ya Patano la
Usharika wa Likamba Kanaisa la KKKT la Wilaya ya Arumeru, Arusha mara tu baada
ya kuuzindua. Wakishuhudia kutoka kulia ni Mfadhili na mlezi wa kwaya hiyo Bw.
Philip Makini, ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa jumuia ya Afrika Mashariki,
akifuatwa na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Makampuni ya IPTL/PAP Bw. Sylvester
Joseph akifuatwa na Bi.Hellen Zelothe.
Moja wa
waumini katika Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba iliyopo Wilaya ya Arumeru
mkoa wa Arusha, Bw. Thedayo Zelothe (kulia) akitoa mchango wake wa fedha pamoja
na jogoo wawili wakato wa harambee ya kuchangia kwaya ya Patano la kanisa hilo
mwishoni mwa wiki kwa lengo la kurekodi albam ya nyimbo za injili. Aliyebeba
majogoo ni Mgeni rasmi katika harambee hiyo ambaye ni Katibu na Mshauri Mkuu wa
Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan
African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege. Wakishuhudia
ni Mfadhili na mlezi wa kwaya hiyo Bw. Philip Makini (wa pili kulia), Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CCK) Bw. Renatus Mwabih (wa pili kushoto) akifuatwa
Bi.Hellen Zelothe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...