Katibu wa Tume ya
Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano
la maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume hiyo
tangu kuanzishwa kwake ambapo Kongamano hilo litawahusisha Mawaziri, KatibuMkuu
Kiongozi na Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea,Taasisi
na Mashirika ya Umma. Kulia ni Naibu katibu wa Tume hiyo Bi NeemaTawale.
Katibu wa Tume
ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano
la maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume hiyo
tangu kuanzishwa kwake ambalo litafanyika
katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere tarehe 30 Oktoba, 2014 ambapo Mgeni Rasmi
anatarajiwa kuwa Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania. Kushoto ni Naibu Katibu wa Tume hiyo Bi Rose Elipenda na kulia ni Naibu
Katibu Bi Neema Tawale akifuatiwa na Naibu
Katibu Bi Rose Mboya. (Picha na Frank
Mvungi-MAELEZO)
Frank Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kongamano la maadhimisho ya Miaka
10 ya Tume ya Utumishi wa Umma yatakayofanyika
jijini Dar es salam Oktoba 30 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi
Claudia Mpangala wakati wa Mkutano na waandishi wa habari ulio lenga kutoa ufafanuzi
kuhusu maadhimisho hayo.
Akifafanua kuhusu siku hiyo Mpangala amesema Kongamano
hilo la siku moja litaanza saa 2:00 asubuhi hadi 11:00
jioni ambapo pamoja na mambo mengine kongamano hilo litahusisha historia ya Utumishi
wa Umma kabla na baada ya Uhuru.
“Kauli mbiu katika
maadhimisho hayo ni Imarisha Uzalendo,Uadilifu na Uwajibikaji katika Kusimamia
Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma ili kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini”
alisemaMpangala.
Akizungumzia wageni watakaoshiriki Mpangala amesema kongamano
hilo litawahusisha Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Watendaji Wakuu kutoka katika
Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Idara zinazojitegemea,
Taasisi na Mashirika ya Umma, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakuu wa Idara ya
Utawala na Rasilimali Watu.
Pia Mpangala alitoa wito kwa waalikwa wote kuhudhuria kongamano hilo kwa lengo la kuonaTume ilipotoka,
ilipo na inapoelekea kwa kuyatazama mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha
miaka 10 na mwelekeo wa Tume katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Tume ya Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu
cha 9 (1) cha sharia ya Utumishi wa Umma NA. 8 ya mwaka 2002 ambapo kwa mujibu wa
kifungu cha 9 (3) cha sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
kwa sharia Na 18 ya mwaka 2007.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...