Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake kutoka RAS Pwani akijitahidi kukaza mwendo katika mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya fedha mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka RAS Pwani, Agatha Gambi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake kutoka Uchukuzi Johari Moshi akimalizia mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia) akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka Uchukuzi, Johari Moshi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanaume za SHIMIWI kutoka Ikulu John Fataki akiwasili kituo cha mwisho cha mbio hizo cha Lake Oil kutoka kituo cha njia panda ya Mkata mjini Morogoro leo.Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...