Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kufua umeme ya TANASI, William
Crawford (mwenye tai ya blue), akimtambulisha mjukuu kwake Colin Machamsoc kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, mara baada ya kuwasilia Wizarani hapo
walipotembelea Leo Asubuhi kutaka kufahamu fursa zilizo za uwekezaji katika Wizara ya
Uchukuzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, akisisitiza jambo kwa kundi la wawekezaji
kutoka nchini Marekani waliotembelea Wizara hiyo leo asubuhi, kutaka kufahamu fursa za
uwekezaji katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi, wawekezaji hao wameonyesha nia
ya kuwekeza katika miradi ya Viwanja vya Ndege, Bandari pamoja na reli.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa
Wizara ya Uchukuzi, Bw. Aunyisa Meena, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa
uliowakutanisha wawezekezaji kutoka nchini Marekani waliotembelea Wizara ya
Uchukuzi leo asubuhi kutaka kufahamu fursa za uwekezaji zilizo katika sekta ya
Uchukuzi.
Robert Shumake kutoka Kampuni ya Shukame Rails akikabidhi mchoro wa Treni
za mwendo kasi Diesel Multiple Unit (DMU) ambazo inataka kuwekeza katika sekta ya Reli kwa
Dkt. Shaaban Mwinjaka, wakati alipomtembelea Wizarani kwa ajiili ya kuangalia fursa za
kuwekeza katika sekta ya Uchukuzi. Kampuni hiyo iko kwenye hatua za mwisho za kusaini
Memorandum of Understanding (MoU) na Shirika la Reli Tanzania (TRL), kwa ajili ya
kutengeneza treni hizo zitakazosafirisha abiria kati ya 800 mpaka 1000.
Afisa
kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), Bw. Ntandu
Mathayo (mwenye shati jeupe), akiwaonyesha wawekezaji kutoka nchini
Marekani, gati namba 1 mpaka 7 inapoanzia katika bandari ya Dar es
Salaam leo asubuhi wakati wawekezaji hao walipotembelea bandari ya Dar
es Salaam kuangaliza fursa za uwekezaji katika bandari ziizoko.
.jpg)
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu wa Mamlaka ya Usimamizi wa BAndari
Tanzania, Mhandisi Alois MAtei, akiwaonyesha wawekezaji kutoka nchini
Marekani, eneo la Bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi walipotembelea
Bandari ya Dar es Salaam kuona fursa za kuwekeza katika sekta ya
Uchukuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...