Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
 Nchi za Zambia, Tanzania na Kenya zimesaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme (ZTK) na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika. 
Akiongea katika hafla hiyo Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, mradi huo wa pamoja unalenga kuondoa tatizo la upungufu wa nishati ya umeme baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika jambo ambalo litachangia katika kukuza uchumi wa mataifa hayo. 
Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia , Christopher Yaruma ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo sio tu utaziwezesha nchi hizo kufanya biashara bali pia utafungua fursa za uwekezaji na kusaidia katika kuondoa umaskini miongoni mwa nchi wanachama kutokana kuzitumia fursa mbalimbali zinazotokana na nishati ya umeme. 
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir amewataka washirika wa maendeleo kusaidia katika kuwezesha utekelezaji wa mradi huo wa kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme baina ya nchi hizo kutokana na manufaa yake kwa bara la Afrika na kuongeza kuwa, kutokana na uwepo wa rasilimali asilia za kutosha katika nchi hizo hakuna sababu ya kuwepo tatizo la nishati katika nchi hizo na barani Afrika.
 Naye Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Soko la pamoja la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi (COMESA), Dkt. Kipyego Cheluget amezipongeza nchi hizo kwa kuuendeleza utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua kipindi kirefu na kuueleza kuwa, ni miongoni mwa miradi 16 ya kipaumbele na kimaendeleo kwa Afrika. 
Aidha, kwa upande wao Washirika wa maendeleo waliohudhuria hafla hiyo, wameonesha kufurahishwa kwao na dhamira ya nchi hizo na kuahidi kushirikana na nchi hizo kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Miongoni mwa washirika wa maendeleo waliohudhuria ni pamoja na uwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank(AfDB) na Ubalozi wa Ufaransa.
 Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaam leo na Waziri wa Nishati na Madini Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto)  na  Waziri wa Nishati na Petroli Kenya , Davis Chirchir (kulia) . Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Migodi , Nishati na Maendeleo ya Maji Zambia, Charity Mwansa, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini , Tanzania , Eliakim Maswi na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Petroli Kenya,  Mhandisi Joseph Njoroge.
 1.      Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo mara baada ya kusaini.
 1.     Mawaziri wa wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo  Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kusaini.
1.     Sehemu wa wadau waliohudhuria hafla ya kusaini Mkataba  wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mbali na Wataalamu kutoka katika nchi hizo, hafla hiyo imehudhuriwa uwakilishi wa COMESA,  Mashirika ya Umeme kutoka nchi hizo na  baadhi ya washirika wa Maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank (AfDB), Ubalozi wa Ufaransa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nchi hizi zimepiga hatua kwa kusaini mapatano haya, jengeni miundo mbinu ya pamoja ya kusambaza umeme ili tujikimu kwa nishati siku za usoni. Tulikotoka ambapo uwekezaji katika miundo mbinu wa umeme haukufanyika hakukuwa kuzuri kimaendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...