Na Andrew Chale

USIKU maalum wa kuenzi vazi la Khanga na magwiji wa taarab nchini 'Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab' unapotarajia kulindima usiku wa leo Novemba 29 ndani ya Ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B, karibu na daraja la Kawe, na kusindikizwa na gwiji wa mipasho Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi. 
Kwa mujibu wa Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin amebainisha kuwa kwa ushirikiano wa Fabak Fashions na Safari Carnival wameandaa usiku huo maalum kuenzi vazi la Khanga.
"Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab ni maalum kuenzi vazi hili la khanga ambapo pia watu wote watakaofika watavaa vazi maalum la khanga. Hivyo wadau wajitokeze kwa wingi kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P." alisema Asia Idarous Khamisin.
Aidha, alisema wadau watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi.
Amesema  leo usiku  pia kutakuwa na zulia jekundu  (Red Carpet)  ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maarufu watakaojitokeza, ambao pia The Legend Dj John Dilinga wa nIsumba Lounge atasimamia muziki Old School.
Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Anko

    Sina nia ya kuchafua hewa lakinikuna huyu jamaa anayejiita legend DJ.Ingependeza angejiita Legend DJ wa madogo kwani kama yeye ni legend Pantalakis,Joe Holela,Seydou,Jerry Kotto,Super Deo,Ebonite Wooljack,Kalikali,Masoud Masoud, hata kizazi cha kina Dillon,Bonny Love,Young Millionea watajiiita kina nani ?
    Awe na heshima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...