Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Ghaith Alghaith, Mtendaji Mkuu na Rais wa Shirika la Ndege la FlyDubai katika ofisi za shirika hilo. Katika mazungumzo, Mhe. Omar Mjenga, amemueleza kuhusu maombi ya Serikali ya Tanzania kwa shirika hili ya kuingia ubia na Air Tanzania kwa ajili ya safari za ndani (domestic flights) na zile za kikanda (regional fligjts). Nia ya mpango huu ni kuiwezesha Air Tanzania kuanza safari zake zote za ndani na kikanda zilizosimama kwa kukosa ndege za kufanya safari hizo. Hivyo basi ushirikiano utakuwa ukiitwa: Air Tanzania Operated by Flydubai. Kwa mpango mashirika yote yataingia mkataba wa kugawana mapato kwa asilimia watayokubaliana.
Balozi Mdogo wa Tanzania -Dubai,Mhe. Omar Mjenga akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Flydubai Mhe. Ghaith Alghaith katika ofisi za flydubai.
Balozi Mdogo wa Tanzania -Dubai, Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Ghaith Alghaith, Mtendaji Mkuu wa shirika la ndege la Flydubai ambalo limezindua safari zake kati ya Dubai na Far es salaam kuanzia tarhe 16 Oktoba 2014 kwa nauli ya dola 399 Dubai-Dar-Dubai. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. my favourite Ambassador mdogo, the guy is always in the news! I love it!

    ReplyDelete
  2. hii habari murua kampuni yetu ya ndege ipate mbia. michuzi muulize mhe balozi limefikia wapi hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...