Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro akiongoza gari ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye kijiji cha Elang’atadapash wilayani Longido kuzindua mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na UNDP.
Na mwandishi wetu
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka wananchi wa Longido kwa kushirikiana na viongozi wao kutunza vyanzo vya maji katika wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yanafanya maeneo mengi kuwa makame.
Alvaro alisema hayo wakati akizindua mradi mkubwa wa maji wa kwa vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash uliosaidiwa na UNDP ambao unahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Mratibu huyo alisema kwamba utunzaji wa vyanzo vya maji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 92 utawezesha wanawake kuendelea kushiriki katika kazi nyingine za jamii badala ya kuhangaika kutwa kusaka maji.
Aidha alisema viongozi wanatakiwa kuendelea kutoa elimu wa kutunza vyanzo vya maji na mradi huo ili uwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akiongozana na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (kulia) mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Elang’atadapash tarafa Kitumbeine wilaya ya Longido mkoani Arusha kuzindua mradi mkubwa wa maji uliosaidiwa na UNDP ambao utahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...