Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufungua rasmi Mkutano wa Tano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Days Hotel & Suites Shinei Bay Mjini Haikou Jimboni Hainan.
Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian Dingzhi akitoa neno la makaribisho kwa wajumbe wa mkutano wa Tano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika unaoendelea katika ukumbi wa Kimataifa wa Days Hotel i& SuitesShiney Bay Mjini Haikou.
Meya Wa Manispaa ya Zanzibar Mstahiki Khatib Abdullrahman Khatib kulia pichani na kushoto yake Mwakilishi wa Jimbo la Chanani Mh. Ussi Jecha Simai wakiwa makini kufuatilia Hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tato wa Kimataifa wa Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Katika Mji Mkuu wa Jimbo la Kisiwa cha Hainan – Haikou.
Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tano wa auashirikiano kati ya China na Afrika, waliopo mbele wane kuanzia kulia ni Meya wa Manispaa ya Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib,Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mh.e Ussi Jecha Simai, Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban,Waziri wa Habari Mh. Said Ali Mbarouk na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.
Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari wa Jimbo la Hainan wakipata ufafanuzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Tano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kutoka kwa Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Mkutano huo Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarBalozi Seif Ali Iddi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...