Katika
mazungumzo maalum na Kituo cha Mlimani TV cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amewasisitiza waandaaji wa matamasha na mashindano ya Sanaa na urembo kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo katika kuendesha matukio yao.

Pia,amewataka waandaaji wa mashindano na matamasha katika vitongoji kuwa makini katika kusimamia taratibu kwani ndiyo wanaoandaa washiriki ambao baadaye wanakuja kushiriki kwenye ngazi ya taifa. 

Katika hili amewataka kutumia upembuzi yakinifu kabla ya kuruhusu washiriki ama wasanii kushiriki katika matukio yao ili kukwepa aibu kwa taifa.

"Kama kuna vielelezo au nyaraka zinahitajika, waandaaji lazima waziombe kwa washiriki na wazihakiki kikamlifu. Kama kuna utata wahakikishe wanahusisha mamlaka zinazohusika mapema ili kuupata ukweli" aliongeza Mngereza.

Aidha, amesisitiza kwamba BASATA litaendelea kuwabana waendeshaji/waandaaji wa matukio ya Sanaa kwani ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na ndiyo wanaopewa idhini ya uendeshaji na Serikali.

“Kama katika ngazi ya vitongoji,wilaya na kanda waandaaji wangeweka msisitizo, changamoto zisingekuwepo. Kuna ulegelege wa kudhibitiwa” Aliongeza. 

Amewataka waandaaji wote kusimamia kanuni  na taratibu zao  kwa haraka pasipo kusubili mashinikizo na malalamiko kutoka kwa jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. BASATA mmeamka kuvuta shuka asubuhi baada ya sakata la hivi karibuni? Mbona mnakuwa wepesi kuwafungia wasanii wanapotoa kazi zao mnazoona haziendani na maadili, lakini wanapoibiwa kazi zao wasanii hatuoni matamko yenu? Ina maana vitendo hivyo viko nje ya uwezo wenu? Kama ni hivyo, nani anayetakiwa kunyooshewa kidole?

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...