Jumla yaVijana 150 kutoka ndani na nje ya nchi wameudhuria Kongamano la Biashara kwa Vijana lililofanyika jijini Arusha ambapo Benki ya CRDB wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wa kongamani hilo.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na Vijana kutoka katika Vyuo Vikuu vya nchi za Afrika Mashariki na kuandaliwa na Taasisi ya AIESEC ambalo hujihusisha na ubunifu wa vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Hall CDTI- TENGERU, Arusha ambalo lilihudhuriwa na wanafunzi 150 kutoka nchi tofauti za kimataifa na 150 kutoka vyuo vya elimu ya juu ndani ya Tanzania.
Benki ya CRDB kama miongoni mwa makampuni yaliyodhamini kongamano hilo, ilialikwa kuweza kutoa elimu juu ya “Teknolojia na Ubunifu” ambapo Mkurugenzi wa mikakati na ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini aliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi walengwa.
Katika kongamano hilo washiriki walipata nafasi ya kuelemishwa kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya kieletroniki zilizotolewa na Mangire Kibanda (Meneja huduma za kibenki kwa njia ya kielektroniki) ambaye alitoa elimu kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya simu (SimBanking), kwa njia ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos), Wakala wa Benki (FahariHuduma).
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada kuhusu teknolojia na ubunifu.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akijibu maswali ya wanafunzi.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Alma Ally (kushoto) akifafanua jambo kuhusu akaunti ya Scholar ambayo ni maalumu kwa wanafunzi.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...