Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ambaye ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akitoa nasaha zake kwa washiriki wa Bonanza hilo lililofanyika leo Novemba 15,2014 kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Picha zote na Othman Michuzi.
Kaimu Mkurugeni wa Elimu na Huduma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Allan Kiulla (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi lililofanyika leo kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Bonanza hilo lililogeshwa kufanyika michezo mbali mbali,ikiwepo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na mingine mingi.Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo.

Kikosi kazi cha Michuzi Media Group  ambayo ndiyo official media kwenye tukio zima la Wiki ya Mlipa Kodi kikiwa tayari kuingia kazini kwenye bonanza la ufunguzi  wa wiki hiyo ambayo  kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti".
Mtanange wa kukata na shoka kati ya Timu ya TRA na timu ya NSSF ulipigwa katika Uwanja wa TCC Chang'ombe,Mtanange uliowatoa kifua Mbele vijana wa NSSF kwa Mabao 4-2 dhidi ya wenzao wa TRA.
Mbio za kuku kwa kina Baba zilikuwa ni sehemu ya michezo iliyofanyika leo Uwanjani hapo.


Vijana wa Kundi la Wanne Star wakionyesha makeke yao mbele ya wadau wa TRA waliofurika kwa wingi kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...