Nani kasema Old School ni kwa muziki peke yake? Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Nathan Chiume na mai waifu wake wanakupa jibu la swali hilo wakiwa katika mfano wa studio za mpiga picha maarufu wa miaka ya sitini wa jijini Bamako, nchini Mali, Malick Sidibe, iliyo katika kituo kipya cha utamaduni wa Afrika (The Africa Centre: BOFYA HAPA) katika barabara ya tano na ya 110 (Fifth Avenue and 110th street) kitongoji cha Manhattan hapo jijini New York kilichoanzishwa na bilionea Mo Ibrahim
Hapo Nathan na Mai Waifu wake wanaonesha mapozi ya wapendanao walipokwenda studio hiyo. Yaani bila kuwa na redio, baiskeli ama pikipiki studio kulikuwa hakunogi. Hehehe...si mchezo enzi hizo. Namna ya kuliingiza na kulitoa hilo bodaboda humo studio ni hadithi ingine. Kwa leo furahia taswira hizo huku ukijiuliza kuna ubaya wa kurudia huko?
Safi saaana. Nathan pinch imetoka ka vile enzi zile.
ReplyDeleteMe Love this!
ReplyDelete