Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru  Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliyeongoza mapokezi hayo ya Ikulu 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. anakuja kukutana na maroroso ya escrow,iptl, tanesco. yani mi sina ham na tanzania, wacha niendelee kubeba box huku ukerewe.

    ReplyDelete
  2. Welcome home Mr. President...sasa wachape wote hao wanaotuharibia nchi yetu na tamaa zao zisizoisha. Washenzi sana na wanajifanya wajuaji kuliko wewe.

    La pili, akirudi Chef Issa, apokelewe hivi hivi, kwa shangwe, maua, press conference hapo hapo alipokaa Mheshimiwa Rais, na Nyalandu, waziri ya mambo ya ndani, waziri wa utamaduni, waziri ofisi ya Rais, n..k. wote waende kumlaki. He is our pride and at the moment tunahitaji sana kitu na mtu wa kujivunia sisi watanzania. Naipenda nchi yangu sana sana. Ndoto yangu kubwa ni kuitumikia, lakini kwa sasa, na hao mafisadi, sitaki kufanya kazi nao. Mungu Ibariki Tanzania yetu!

    ReplyDelete
  3. This happened to me, a key hole operation was done on a Friday, and Monday was back to work. It's curable cancer if detected early. But as a president of a country, I admire him how he went through long meetings and also the lack of sleep due to constant toiletting. Pole sana mr president, I hope it is all sorted out.

    ReplyDelete
  4. Karibu home and please clean up the cabinet, our country is basically rotten with corruption.

    ReplyDelete
  5. Karibu nyumbani Dr. JK. Nimeshukuru Mungu amekupa neema na afya njema na unaweza kurudi kulitumikia taifa. Nina maombi mawili kwako unavyoigusa ardhi ya tanzania baada ya wiki mbili au tatu huko majuu:

    (a) watoto wetu wanshindwa kwenda shule. Sababu:escrow
    (b) watoto wetu, wazazi wetu hawajala leo mchana na hawajui watakula nini leo jioni (walikunywa chai ya rangi leo asubuhi) Sababu:escrow
    (c) leo hii wale watu kule dar es salaam wenye uwezo walikuwa wameweka nyama kwenye friji, lakini umeme ulukatika tangu juzi na nyama yote imeharibika: Sababu:escrow
    (d)Uwongo mwingi sana uliendelea kwenye bunge tukufu wakati haupo: pesa zetu za kodi huko tanesco tuliambia si zetu; wengine walisema kwamba wewe unawaogopa viongozi uliowateua mwenyewe; kiongozi mkuu wa bunge (linalosimama kama mhimili pekee) ameogopa kutoa maamuzi magumu; na utumbo mkubwa uliotokea huko dodoma wakati haupo: Sababu:escrow
    (e) na sasa umekuja nafikiri wote waliofikiri wewe umekaa kimya tu watakiona hasa wale walioshikwa kwa sababu ya escrow!
    Waonyeshe kwamba umerudi na nguvu mpya, uwezo mpya na mawazo mapya!
    Mungua akuongoze katika maamuzi utakayofanya wiki inayokuja, na miezi michache ijayo. Ninakutakia maisha mema! Amen
    Mimi mtanzania ninayeililia tanzania yangu!

    ReplyDelete
  6. Ujio wa mama nyerere kiwanja cha ndege umebeba ujumbe mzito mno yataka tafakari ya kina kugundua hilo....

    ReplyDelete
  7. Ujumbe wa Mama Maria ulikwa simple. Mr. President nchi imeoza, tafashali iokoe nchi la sivyo mamabo yataenda mrama.

    ReplyDelete
  8. Anonymous wa Tarehe 30 Nov nakushukuru kwa ujumbe wako wa kumkaribisha JK nyumbani vizuri. Sote tunamtakia afya njema.

    Ijapokuwa ujumbe umesema kwamba una maomhi mawili inaonyesha una maombi zaidi ya moja. Ni vizuri tu. Tunatumaini atayapokea yote hayo naye JK atachukua uamuzi mgumu sana hivi au hivi karibuni! Zaidi ya yote,muheshimiwa Rais JK tunakuomba umwambie mama Makinda kwamba yeye pia ni mkuu wa mhimili mmoja kati ya mitatu na mhimili wake unajitegemea (bunge), na kwa hiyo yeye pia ana uwezo wa kufanya maamuzi magumu kama na wewe unavyofanya au jaji mkuu anavyofanya. Juzi ijumaa alionyesha kutapatapa katika kazi hii na hakuonyesha uwezo wa kufanya maamuzi magumu!

    Wakati ninakusubiri ufanye maamuzi magumu, ninaendelea kukuombea kwa Mungu akupe afya njema wewe na familia yako yote

    Wasalaam, mimi ni Mtanzania halisi

    ReplyDelete
  9. Wewe mtoa maoni wa mwisho umesema kitu ambacho hatukifikiria.Ujio wa Mama Nyerere una ujumbe mzito sana, jua kwamba hata mama huyu hajafurahia tendo hili la ajabu liliikumba Tanzania. Mungu tuoneshe njia, tunaipenda sana Tanzania ijapo wako watu wachache sana wanaoiharibu Tanzania. Hata CCM kama chama si chama kibaya ila watu walioko humo ndo wanakichafua hicho chama. Mheshimiwa Rais tulia na omba kwa Mungu ufanye maamuzi yenye haki.

    ReplyDelete
  10. Bola jk umerudi sasa kilichobaki ni kuwachinjia baharini hao wezi, pia tunasubili utoe amri ya kufilisiwa mali zao ili iwe fundisho, tunakupenda rais wetu

    ReplyDelete
  11. I think bongo we have to start respecting public monies and property, watu wanazoa tu na ku share as if they are entitltled to it. These are professors!

    ReplyDelete
  12. Wasio na uzalendo wameonekana na walio safi wamepambuka. Tunachohitaji Watanzania ni nchi yetu inayoendelea. Wakio wenfi wanasahau cheo ni dhamana.!

    Kila aliye na uwezo wakuomba na kuonyesha tuoneshe. Wale walio na dhamana muitunze amana mlo nanyo mkononi. Zito Kabwe na team hongera na wale Mafisadi wateketee. Muheshimiwa Rais na wote wahusika munayo amana mkononi. Hao walaji kwenye Serikali na hata Mashirika ya dini SI WENZETU. Tumeshawajua na HATUWATAKI. Kama wasomi wako wengi TZ. Wapeni dhamana kutuongoza kwenye maendeleo na siyo kutudidimiza. Yetu ni maneno matendo mnayo wenye DHAMANA. Mungu ibariki Tanzania na utulindie nchi yetu, Amen.

    ReplyDelete
  13. Hatutaki maneno tunataka vitendo. Kama wamechukua fedha za ymma WAZIREJESHE. Hatutaki utetezi tunataka vyetu wa TZ. Hata huko kwenye machafuko huanza hivihivi. Jamani ondokeni murudi mlikotoka. Wengine hawafai hata kurudi Chuo kikuu walikokuwa wanafundisha. Na kwa upande mwingine wanadhihirisha walivyokuwa wanawaonea hao walokuwa wanawafunza. Labda hata walikuwa wakiuza mitihani. Kiongizi wetu waondoe tafadhali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...