Sophia Yona mwanadiaspora wa New York akiuliza jambo kwa mwakilishi wa Exim Bank Bwn. Dinesh Arora kwenye Career Africa iliyofanyika jiji lisilo lala New York City ndani ya hotel ya Hilton iliyopo mtaa wa 1335 avenue of America, New York New York 10019 na wanaDiaspora takribani 400 walijitokeza kwenye Careear Africa hiyo iliyokua imeandaliwa na baadhi ya wana Diaspora wa New York na New Jersey kwa kushirikiana na makampuni makubwa yanayofanya shughuli zake Afrika yaliyofanya kongamano hilo kwa ajili ya kuwatafuta wanaDiaspora wa Marekani wanaopendelea kufanyakakazi kwenye makampuni yao. Makampuni yaliyoleta wawakilishi  ni AXA insurance, Exim bank, national Microfinance Bank (NMB). OCP group, PZ Cussons, Safaricom na Tollow Oil.
Bi. Rokyaya Mane (kulia) mwakilishi wa National Micfofinance Bank (NMB) akitoa maelezo kwa wanaDiaspora waliohudhuria kongamano hilo lililoandaliwa maalum kutafuta wanaDiaspora wanaopendelea kuajiliwa na makampuni hayo Kongamano la Career Africa lililofanyika kuanzia Ijumaa Novemba 7-9, 2014 jijini New York City.
Bwn. Alaoui Banachem (kulia0 mwakilishi kutoka OCP Group akitoa maelezo kwa mwanaDiaspora huku akijaribu kuinadi kampuni yake kwa madau.
WanaDiaspora waliohudhuria kongamano la Career Africa wakibadilishana mawasiliano.
Kushoto ni Bwn. Frederick Kanga mwakilishi kutoka Exim Bank akisalimiana na mwanaDiaspora aliyetembelea meza hiyo kujaribu kupata mawili matatu.
WanaDiaspora wakipata mawasiliano na kuuliza maswali kwa makampuni yaliohudhuria Career Africa jijini New York. 

kwa picha zaidi Bofya Hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kwani Bongo kazi ni benki peke yake ?

    ReplyDelete
  2. They need to hire people back home thousands of University graduates don't have jobs some have been waiting for more than 3 years. People in USA have more opportunities than their fellows back home it doesn't make no sense to recruit people in USA. These Banks waste money to send these recruiter to USA instead of hire bright Tanzanian to boost the economy.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...