DAKTARI,
Assay Shibanda(kushoto) na John Yuccas wakimwekea mwanafunzi wa Shule
ya Msingi Elbol,Levina Innocent mashine ya kuongeza kiwango cha usikivu
kwenye Kliniki inayoendeshwa kwa pamojakati ya Montage Limited na
taasisi kutoka Marekani ya Starkey Hearing Foundation ya kuwawekea vifaa
vya kuongeza usikivu inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo
Palace jijini Arusha jana
Mtaalamu
wa matatizo ya usikivu kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya
nchini Marekani, Derek Johson akimfanyia uchunguzi wa awali wamasikio
mmoja wa watu wenye usikivu hafifu waliokuja kuhudhuria Kliniki
inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana
Mratibu
wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation kutoka Marekani, Derek Johnson
akitoa maelezo ya awali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na
chuo cha Biashara cha Arusha, (IAA) waliokuja kujitolea kutoa huduma
mbalimbali ya matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwangocha usikivu
masikioni kwenye Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo
Palace jana. Kushoto ni Msimamizi Mkuu wazoezi hilo, Teddy Mapunda.
MMOJA wa wataalamu wa kuchunguza matatizo ya masikio,Stuart Specer kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani inayoendesha kliniki ya masikio aakitaniana na mkazi wa Arusha,Ally Abdulrahman aliyewahi kuishi nchini humo ambaye kwa sasa ana matatizo ya kusikia kwenye kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo PalaceJijini Arusha jana

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...