Michuano ya DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP imeendelea leo kwenye uwanja wa Bandari maeneo ya Tandika Mwembe Yanga kwa kuzikutanisha timu za TEMEKE MARKET na BLACK SIX
ya Buguruni,mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kushindwa kumpata
mshindi baada ya kufungana bao 1-1 baada ya dakika tisini,na pia
ilipofika changamoto ya mikwaju ya penati timu zote zilitumbukiza
mikwaju yote mitano kimiani na kupelekea mwamuzi wa mchezo huo kuuvunja
baada ya giza kuingia.
Mchezo huo sasa utarudiwa siku ya jumanne ya tarehe 18/11/2014 kwenye
uwanja huo huo wa Bandari.
Robo Fainali ya tatu inaytaraji kupigwa kesho kwenye uwanja huo huo wa
Bandari kati ya Burudani FC ya Temeke Mikoroshini dhidi ya Kiluvya UTD
kutoka mkoani Pwani.
Mashabiki wakishuhudia mtanange wa TEMEKE MARKET na BLACK SIX ya Buguruni kwenye DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP.
Mpambano ulipigwa kwenye dimba la Bandari maeneo ya Tandika Mwembe yanga.....




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...