![]() |
Marehemu Omar Ndege Mgori |
Familia ya Mzee Ndege inatoa shukurani nyingi kwa ndugu, jamaa marafiki ma majirani waliokuwa nao bega kwa bega tokea ndugu yao mpendwa Marehemu Omar Ndege Mgori kilichotokea mwezi wa jana huko India na hatimaye kuzikwa siku ya jumatatu Oktoba 13, 2014 kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Familia inasema haina cha kuwalipa zaidi ya AHSANTE SANA na kumuomba Mola awajazie pale palipopungua.
Dua maalumu ya kumuombea Marehemu Omar Ndege Mgori imepangwa kufanyika siku ya tarehe 23 mwezi huu, huko Mbezi jijini Dar es salaam nyumbani kwa marehemu kuanzia saa sita mchana. Familia inawakaribisha ndugu, jamaa, marafiki na majirano wote siku hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...