Hii ndio ile barabara ya Ukonga Mazizini- Moshi Bar ambayo inadaiwa kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 90 kuikarabati kwa kiwango cha changarawe kwa umbali wa kilometa tatu. Picha hizi ni madimbwi ya mwanzo tu ya hizo kilometa tatu.(Picha na Father Kidevu Blog).
Meya Jerry Silaa wa Ilala ambaye ni Diwani wa Gongo la Mboto alipotembelea aliwaambia wananchi kuwa fedha za ujenzi huo ni kutoka mfuko wao ni . PICHA ZA CHINI NI SIKU MEYA SILAA ALIPOTEMBELEA UJENZI WAKE.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibarkilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi yadharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huoambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tabia inanikera hii ya kuchimbuachimbua sijui ndio nini...kuwapa tabu bure binadamu wenzenu....sasa ndio nini???ujenzi???au uharibifu wa mazingira???

    ReplyDelete
  2. Milioni 90 ? Wizi mtupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...