Idadi ya wanaojiunga nayo yazidi kuongezeka


Kulwa Saiduni wa Bombo,mkoani Tanga ni miongoni mwa maelfu ya watanzania wanaoweza kupata taarifa zinazohusu afya katika hali ya utulivu wakiwa majumbani mwao.Hii inatokana na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kuanzisha huduma ya Simu Dokta ambayo inawawezesha wateja wake waliojiunga na huduma hii kupata taarifa za afya kupitia simu zao za mkononi.

Hii huduma ni ya aina yake kuanzishwa nchini Tanzania ikiwa inatolewa na Vodacom.Inashirikisha madaktari bingwa wa fani mbalimbali  ambao wamejitolea kutoa utaalamu wao kuhusiana na masuala ya afya na taarifa hizo zinawafikia watanzania kwa njia ya mtandao wa simu popote walipo nchini.

Kulwa, kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mwili ambayo amekuwa hakijitibia kwa muda mrefu bila kupona.Hivi sasa amepata nafuu ya ugonjwa huu baada ya kupokea ushauri wa kitaalamu kupitia huduma ya simu dokta “Sikuweza kumudu kumuona daktari bingwa wa ugonjwa uliokuwa unanisumbua kwa muda mrefu,nimepata ushauri ambao umenisaidia kupitia huduma ya simu dokta.nimebadilisha vyakula ,natumia zaidi matunda na mboga za majani na hali yangu imebadilika kwa haraka naendelea vizuri”.Alisema.
Huduma ya simu Dokta ilizinduliwa rasmi tarehe 4,Novemba ambapo mbali na kutumika kupata taarifa za afya kutoka kwa wataalamu pia inamuwezesha mtumiaji wake kupata taarifa za madhara ya kiafya yasababishwayo na mtindo wa maisha wa mtu pia masuala mbalimbali yanayohusiana na afya kwa ujumla.Kupata huduma mteja akijiunga anakatwa shilingi 100/-kwa siku,ambapo mteja huweza kupata jumbe zipatazo mbili au zaidi kuhusiana  na masuala ya afya.

Kama ilivyokusudiwa huduma hii imekuwa msaada kwa jamii za watu wanaoishi maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa taarifa maeneo hayo ni mgumu pia huduma hii inakidhi juhudi za serikali kufikia malengo ya millennia ambapo lengo mojawapo namba 6 ni kukinga na kuondoa magonjwa mbalimbali.Huduma hii inawawezesha watumiaji kupata taarifa kwa wakati kuhusianana magonjwa na jinsi ya kujikinga nayo na kutunza afya zao.

“Sote tunajua kinga ni bora kuliko tiba.Wateja wetu wanaweza kupata taarifa kuhusiana na magonjwa yanayowasumbua kutoka kwa madaktari bingwa ambao wamejitolea kuelimisha jamii kupitia huduma hii na tuna imani wananchi wengi wanaendelea kunufaika nayo”.Alisema Kelvin Twissa,Mkuu wa Masoko na Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania.

Amewataka watanzania kuchangamkia fursa ya kutumia huduma hii na kuongeza kuwa jamii ambayo inapata taarifa za kutosha ni rahhisi kujikinga na maradhi na kuchukua hatua sahihi yanapotokea magonjwa ya dharura.
Twissa aliendela kusema:”Kupata huduma hii  na ushauri kutoka kwa madaktari bingwa mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma neno DAKTARI kwenda namba ya simu 15542”.

Baadhi ya madaktari bingwa wanaotoa ushauri kupitia huduma hii ni pamoja na Dk.Meshack Shimwela,Dk.Sulende Kubhoja ambao ni madaktari bingwa wa  magonjwa ya watoto na moyo na Dk.Munawar ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...